Ni kitu gani maalum kuhusu mahali unapoishi? Je ni ardhi unayoipenda? Tunakisia kuwa uko hapa kwa sababu kuna sehemu fulani ambayo ni muhimu kwako ambayo ungependa kusaidia kulinda - inaweza kuwa ni mto unaoishi kando kando nao, au msitu ambao familia yako imeishi kwa vizazi vingi. Na, kwa bahati mbaya, ardhi zetu zinazidi kuhatarishwa.
Zana hii tumeiuunda ili kusaidia watu wanaofanya kazi muhimu ya kulinda dunia -- hasa wale wanaopenda kutumia ramani, ufuatiliaji au zana ya simulizi za hadithi ili kusaidia kulinda ardhi dhidi ya uharibifu wa mazingira.
Yafuatayo ni baadhi ya maswali na mazoezi ambayo tumeona yanafaa wakati wa hatua za awali za kujenga mradi.
1. Ni nini kinaifanya ardhi/mito/milima/msitu wako kustahili kulindwa?
2. Je, ni matishio gani makubwa zaidi kwenye ardhi yako, na jamii yako?
3. Je, unauwezo wa kufanya mazungumzo na watu wengine katika jamii yako yako ili kuzungumza na kupitia maswali haya na kuorodhesha baadhi ya mawazo yatakayopatikana?
Zoezi moja rahisi la kukusaidia kuanza limechochewa na mbinu ya "mpango wa maisha" (plan de vida) ilianzishwa na jamii za Wenyeji nchini Kolombia. Mpango huu unalenga kupata mitazamo kutoka kwa vizazi vyote -- ikiwa ni pamoja na maoni ya wazee, watoa maamuzi pamoja na vijana. Mpango huu unaweza kufanywa na vikundi vikubwa au vidogo, kwa kuhakikisha uwepo wa maoni tofauti kwenye jamill.
1. Katika ramani ya kwanza, uliza: Eneo la zamani lilikuwa na sura gani? Jadili na chora kama kikundi.
2. Katika ramani ya pili, uliza: Je, eneo linafananaje leo? Jadili na chora kama kikundi.
3. Katika ramani ya tatu, uliza: Tungependa eneo liweje kesho? Jadili na chora kama kikundi.
Kufanya zoezi hili kunaweza kukusaidia wewe na jamii yako kufikiria ni wapi mnataka kuelekeza nguvu zenu.
Neno ambalo unaweza kulisikia sana ni ushirikishi - hii inarejelea miradi ambayo imejengwa kwa njia inayohusisha jamii nzima. Ingawa uchoraji ramani wa kitamaduni unaweza kuhusisha watu wachache tu, katika uchoraji shirikishi kila mtu (ikiwa ni pamoja na vijana na wazee) anahusika katika mchakato wa kutengeneza ramani. Msisitizo huu wa kushirikisha jamii nzima husaidia kuboresha ubora wa ramani na kuhakikisha kuwa inawakilisha mitazamo mingi ndani ya jamii. Eneo la ramani kamwe halipaswi kusemwa na mtu mmoja.
Nini | Je, unajaribu kufikia lengo gani? (Mafanikio yangekuwaje?) Je, unahitaji kukusanya data ya aina gani? Ni aina gani ya usaidizi wa nje unaweza kuhitajika? (Kama vile kiufundi, kifedha, kisayansi, kisheria, upatikanaji wa zana, mafunzo, n.k.) Je, ni aina gani ya kazi/shughuli zitakusaidia kutimiza lengo lako? (Kama vile mikutano, mafunzo, kazi ya shambani, ukusanyaji wa data, n.k) |
Ni | Je, ni nani ataathiriwa na mradi huu? Nani atashiriki? Nani ataongoza mradi huu na kuuweka sawa? Jukumu lako ni lipi? Nani anaweza kusaidia kazi? (Je, wewe ni sehemu ya shirika au shirikisho linaloweza kuchangia wakati au rasilimali?) Je, ungependa kufanya maamuzi vipi kama kikundi? |
Wapi | Je, mradi huu utafanyika wapi? Je, ni baadhi ya vipengele gani mahususi vya mahali hapa ambavyo vitaathiri mradi? Kama vile muktadha wa kisiasa, shughuli za jumuiya zilizo karibu, n.k. |
Lini | Je, ni lini unatarajia kukamilisha mradi huu? (Hata kama unatarajia kuwa kazi kubwa zaidi itakuwa ikiendelea, ni vyema kuweka tarehe lengwa ili kutimiza malengo mahususi na kuhakikisha kuwa mradi unaendelea) |
Kwa | Nini ni hili jambo ni la maana? Ni kitu gani kipo hatarini? |
Teknolojia -- kama vile simuza mikononi, ndege zisizo na rubani, kompyuta na GPS -- pekee haziwezi kulinda ardhi zetu. Tulichojifunza ni kwamba teknolojia inakuwa bora zaidi pale inapojumuishwa katika miundo iliyopo kwa ushirikiano ndani ya jamii.
Teknolojia inaweza kusaidia wakati:
Teknolojia inaweza pia kuleta matokeo yasiyotarajiwa, na ikiwa unatumia teknolojia kukusanya taarifa nyeti, ni muhimu kuchagua zana zinazowezesha jumuiya yako kudhibiti data zako mwenyewe, ili kuhakikisha kwamba haikuweki wewe au watu wako hatarini kimakosa.
Athari chanya zinazowezekana
Athari hasi zinazoweza kutokea